Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza
kifo cha Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu)
kilichotokea tarehe 13 Aprili 2017.
Marehemu Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu)
alizaliwa tarehe 13 Novemba 1944, mtaa wa Uhuru, Tarafa ya Kariakoo,
Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam. Alisoma na kuhitimu Shule ya
Msingi mkoani Dar es Salaam na baadaye kuendelea na masomo ya Sekondari
katika Shule ya Sekondari St. Joseph Convert School, Dar es Salaam hadi
alipohitimu Kidato cha Nne mwaka, 1963.
Marehemu Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu),
alijiunga na JWTZ tarehe 07 Desemba 1964 na kutunukiwa Kamisheni tarehe
22 Juni 1967. Alistaafu Utumishi Jeshini kwa Heshima tarehe 30 Juni
1999.
Katika utumishi wake Marehemu alishika Nyadhifa mbalimbali Ikiwemo
Mkaguzi Mkuu wa Jeshi Makao Makuu mpaka anastaafu. Mwili wa Marehemu
unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 20 Aprili 2017 katika Hospitali ya Jeshi
Lugalo kuanzia saa 10:30 Asubuhi.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment