Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17
‘Serengeti Boys’ imepata ushindi wa magoli 2-1 kwenye mchezo w kirafiki
wa kujipima nguvu dhidi ya Gabon ambao ni wenyeji wa michuano ya AFCON
U-17 2017.
Mechi hiyo imepigwa nchini Morocco ambapo Serengeti Boys imeweka
kambi kwa ajili ya maandalizi ya michuano vijana wa chini ya miaka 17
iyopangwa kufanyika Gabon kuanzia Mei 14 mwaka huu.
Magoli ya Serengeti Boys yamefungwa na Kelvin Nashoni na Ibrahim Abdallah Ally.
Shaffihdauda.co.tz inaungana na watanzania wote kuitakia kila la heri
Serengeti Boys iendelee kujiandaa vyema ili iwakilishe taifa vizuri
katika michuano hiyo ya vijana.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment