Chameleone amekanusha tetesi kwamba mkewe Daniella Atim amekwenda mahakamani kudai talaka.
Taarifa zilisambaa mitandaoni kwamba Daniella alidai kwa kutokuwa na
furaha na ndoa yake kutokana na manyanyaso na vipigo anayoyapata kutoka
kwa muimbaji huyo mkongwe wa Uganda.
Chameleone ameamua kuvunja ukimya kupitia mtandao wa Facebook kwa
kurusha video ya dakika 53 akiongelea mengi kuhusu familia yake, ambayo
inaonekana kuwa na furaha tofauti na yanayozungumzwa.
“Kuna habari nyingi zimesambaa zinazohusu mimi na familia yangu.
Siwezi kusema kubwa lolote lakini nachotaka kusema ni kuwa sina talaka
wa hakuna anayedai talaka,” amesema msanii huyo kwenye video hiyo.
“The beautiful Daniella there. Kumbuka mimi ni mkatoliki, mkatoliki akifunga ndoa hawezi kuachana,” ameongeza.
Ndoa yangu haivunjiki Ng’o!- Chameleone
Title: Ndoa yangu haivunjiki Ng’o!- Chameleone
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Chameleone amekanusha tetesi kwamba mkewe Daniella Atim amekwenda mahakamani kudai talaka. Taarifa zilisambaa mitandaoni kwamba Daniella...
Post a Comment