Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Jah Prayzah azidi kunogewa na Bongo Flava
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Ni dhahiri, Jah Prayzah amenogewa na ladha ya muziki wa Bongo Fleva. Muimbaji huyo kutoka Zimbabwe, anamshukuru Diamond kila kukicha, a...
Ni dhahiri, Jah Prayzah amenogewa na ladha ya muziki wa Bongo Fleva.

Muimbaji huyo kutoka Zimbabwe, anamshukuru Diamond kila kukicha, ambaye alimshirikisha katika wimbo wake wa ‘Wotora Mari’ na kumpatia tobo kubwa Afrika kwa kuanza kusikilizwa zaidi maeneo mbalimbali Afrika, na kupelekea kujinyakulia tuzo ya Listener’s Choice Awards ya MTV MAMA mwaka jana.
Sasa mkali huyo ameonekana akiwa studio na msanii kutoka WCB, Harmonize na kuandika ujumbe katika mtandao wa Instagram unaoashiria maandalizi ya wimbo wao mpya.
“In the studio again with another Tanzanian big star @harmonize_tz .Zimbabwe neTanzania 🔥,” ameandika Jah katika mtandao huo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top