Alianza Willian dakika ya tano tu ya mchezo kuanza kucheka na
nyavu za Tottenham Hotspur kwa mkwaju wa faulu na kuifanya Chelsea
kutangulia kwa bao moja kwa sifuri.
Baadae Harry Kane aliisawazishia Chelsea na watu kuona kama kipindi
cha kwanza kinaweza kuisha kwa sare ya bao moja kwa moja lakini Chelsea
walizawadiwa penati na Willian tena akafunga la pili na kwenda mapumziko
kwa matokeo ya mbili kwa moja.
Kipindi cha pili Delle Ali aliisawazishia Tottenham Hotspur lakini
mabadiliko aliyoyafanya Antonio Conte ya kumuingiza Eden Hazard
yalibadilisha kabisa matokeo ya mchezo huo.
Dakika ya 75 Eden Hazard aliifungia Chelsea bao la tatu kabla ya
kuasist bao la nne lililofungwa na Nemanja Matic na kuufanya mchezo huo
kuisha kwa matokeo ya bao nne kwa mbili.
Kwa matokeo hayo Chelse imetinga fainali ya FA itakayopigwa baadae
mwezi ujao katika uwanja wa Wembley huku wakimsubiri mshindi wa mchezo
kati ya Arsenal na Man City utakaopigwa siku ya Jumapili.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment