Ukata mkubwa wamliza CAG
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wakati kutokana na ukata.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad amesema hayo jana wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanyakazi wa ofisi yake mjini hapa.
Amesema anashindwa kufanya kazi kwa kufikia kiwango cha kitaifa na kimataifa kama inavyotakiwa licha ya kuwa na watumishi wenye ari ya kufanya kazi kwa muda mwafaka.
Alisema “Kingine niseme kuwa, nashindwa kukaa ofisini kwa utulivu kutokana na madeni makubwa ya makandarasi ambao wanajenga majengo yetu, likiwamo la Rukwa, kweli nina shida kubwa.”
By: Emmy Mwaipopo
Chanzo: Mwananchi
Post a Comment