Rais Magufuli atoa salamu za rambirambi kufuatia msiba wa George Kahama
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri wa Mambo ya Ndani, George Kahama.
Hii taarifa yake:
Clement George Kahama ‘Sir George’ (89) amefariki dunia Jumapili katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mtoto wa marehemu, Joseph Kahama amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Alisema kwa ufupi kuwa “Ni kweli. Mzee wetu amefariki dunia saa 10 jioni hapa Muhimbili.”
Msiba wa Kahama si tu ni mzito kwa familia yake, bali pia kwa taifa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa nchi kabla na baada ya Uhuru. Kahama ni mtumishi wa umma aliyekuwa mtendaji mkuu na mwanasiasa aliye mahiri na makini katika utendaji kazi kuanzia nyakati za Tanganyika kudai uhuru miaka ya 1950 hadi kujitawala mwaka 1961, na baada ya Uhuru mpaka alipostaafu utumishi wake.
Kahama alizaliwa Novemba 30, mwaka 1927 na ameacha mke na watoto 11.
Post a Comment