Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Nataka kuwa Beyonce wa Bongo – Nandy
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki kutoka THT, Nandy amefunguka kwa kudai kuwa atahakikisha anafanya vizuri katika muziki anaofanya ili afike mb...


Msanii wa muziki kutoka THT, Nandy amefunguka kwa kudai kuwa atahakikisha anafanya vizuri katika muziki anaofanya ili afike mbali zaidi kama wasanii wakubwa duniani.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘One Day’, amedai msanii akimuomba Mungu, juhudi katika muziki wake pamoja na nidhamu ya kazi anaweza kufika mbali zaidi.
“Nimemweka mbele Mwenyezi Mungu, pia Watanzania waniweke kwenye sala zao. Nimepanga vitu vingi kwenye muziki wangu nataka kuwa zaidi ya mastaa wa kike Bongo, siwezi kuwaangusha naona ndiyo kwanza naanza, nataka kuwa kuwa Beyonce wa Bongo,” alisema Nandy.
Kwa sasa muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii wa kike ambao wanafanya vizuri kwenye tasnia ya muziki nchini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top