MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI ATAHADHARISHA WANANCHI UPATIKANAJI WA MAFUTA ISIWE SABABU YA KUBWETEKA
Msimamizi wa Kampuni itakayofanya Utafiti waUtafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya Bell Geospace Inteprises Limited
Bwana Stephane Kunar kushoto akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia nanma ndege Maalum itakavyofanya
utafiti huo katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar. Kati kati ni Waziri
wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira mhg. Salama Aboud Talib, wa nyuma
yake ni Katibu Mkuu wake Nd. Ali Khalil Mirza na Mkuu wa Mkoa Mjini
Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mhmoud.
Balozi Seif akiangalia baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyochunguza maeneo yenye daliliza uwepo wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.
Balozi Seif akijaribu kugusa vifaa vitakavyotumika katika kazi kufanya utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia sehemu zenye dalili ya uwepo wa Mafuta na Gesi Visiwani Zanzibar.
Baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege Maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyofanya utafiti wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.
Baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege Maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyofanya utafiti wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.
Baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege Maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyofanya utafiti wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametahadharisha
Wananchi kwamba itakapofikia hatua ya kupatikana kwa rasilmali ya Mafuta
na Gesi Asilia Visiwani Zanzibar isijekuwa chanzo cha sababu ya
Wananchi kubweteka na mradi huo kwa kuacha shughuli zao za Kiuchumi
ambazo huwapatia riziki zao za kila siku.
Alisema
Rasilmali hiyo endapo itapatikana kufuatia utafiti unaoanza kufanywa
hivi sasa itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza changamoto nyingi
zinazoikabili Serikali Kuu pamoja na Wananchi kwa ujumla.Balozi Seif Ali
Iddi alitoa tahadhari hiyo wakati wa hafla maalum ya uzinduzi
wa Ndege itakayofanya Utafiti na hatimae uchimbaji wa Rasilmali ya
Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Abeid Aman Karume nje kidogo ya Kusini ya Mji wa Zanzibar.
Alisema
yapo Mataifa mengi Duniani yakiwemo yale ya Bara la Afrika yaliyoanza
kuzalisha miradi hiyo kwa matumaini makubwa ya kuimarisha Uchumi wao
lakini hivi sasa zimekuwa na changamoto zaidi za Kiuchumi hali ambayo
Zanzibar na Wananchi wake wanapaswa kuwa makini na
kujifunza matukio hayo.
Hata
hivyo Balozi Seif alisema safari ya Zanzibar kuelekea kwenye uchumi Mkuu
imeanza mara baada ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitisha Mswaada
wa kuanzisha sheria inayoiruhusu Zanzibar kutafuta na kuchimba mafuta
yake yenyewe na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mainduzi kusaini Sheria hiyo.
Alisema
busara za Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete za kusimamia utaratibu wa kupelekwa mswada
Bungeni zimepelekea suala la mafuta na Gesi Asilia hivi sasa kutoka
katika mambo ya Muungano.
Balozi
Seif alifahamisha kwamba Zanzibar na Wananchi wake wamefarajika na
mwanzo mzuri wa hatua za awali za utafiti na baadaye uchimbaji wa Mafuta
na Gesi Asilia ndani ya mipaka yake ya Visiwa vya Zanzibar. Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Kampuni ya Utafiti na Uchimbaji
wa Mafuta na Gesi Asilia ya Nchini Ras Al – Khaimah { RAK GAS } kwa
juhudi zake zilizoonyesha nia safi ya kushirikiana na Zanzibar katika
Mradi huo mpya wa Mafuta na Gesi.
Alisema
Rak Gas imekuwa mshirikia mkubwa wa Zanzibar katika harakati za
kuwaondoshea dhiki ya huduma za Maji safi na salama Wananchi wa Zanzibar
ambapo tayari Kampuni hiyo imeshafadhili nuchimbwaji wa visima 100
Unguja na Pemba. “ Tumeshuhudia juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali
ya Rais Al –Khaimah Kupitia Kampuni ya Rak Gas katika kuunga mkono
harakati za Kijamii Visiwani Zanzibar ”. Alisema Balozi Seif.
Balozi
Seif aliwataka Wananchi wote kutokuwa na hofu kwa ndege itakayohusika
na utafiti wa Mafuta na Gesi katikia maeneo yanayodhaniwa kuwa na
Rasilmali hiyo kwa vile itaruka katika maeneo ya chini zaidi na kuwataka
waendelee na shughuli zao kama kawaida.
Mapema
Mhandisi Muandamizi wa Kampuni ya Rak Gas kutoka Nchini Ras Al –
Khaimah Dr. Osama Abdd – AAL ameipongeza Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar kwa kuanza kuweka Historia mpya katika muelekeo wake
wa mradi wa Kiuchumi wa Mafuta na Gesi Asilia.
Dr.
Osama alisema Wananchi wa Zanzibar na ndugu zao wa Ras Al – Khaimah
tayari wamekuwa na uhusiano wa Kihistoria uliopelekea
kujenga ushirikiano zaidi katika uanzishwaji wa utafiti wa Mafuta na
GesiAsilia Zanzibar.
Alisisitiza
kwamba utiaji Saini Mkataba wa Utafiti wa Rasilmali hiyo uliofanywa na
Serikali zote mbili Nchini Ras Al – Khaimah karibu miaka miwiliiliyoita
ni uthibitisho wa uhusiano huo wa pande hizo mbili. Naye Msimamizi wa
Kampuni ya Bell Geosace Interrises Limited inayofanya Utafiti huo Bwana
Stephane Kunar alisema ataalamu wa Taasisi hiyo wako makini katika suala
ya uhifadhi wa mazingira wakati wanapoendesha tafiti zao.
Bwana
Kunar alisema hatua hiyo inakuja kutokana na uzoefu mkubwa waliyonao
wahandisi hao kwa karibu miaka 70 sasa tokea kuanzishwa kwake ambapo
Barani Afrika kazi hiyo wanaiendeleza kwa zaidi ya miaka 15 sasa.Alisema
utafiti wao ambaowanaufanya kwa zaidi ya Mita 100 chini ya ardhi pamoja na maeneo ya Bahari kwa Afrika umeshafanyikka Afrikka kwa Nchi ya Botswana Brazil Barani Amerika ya Kusini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
14/3/2017.
Post a Comment