Airtel washirikiana na UCSAF kufikisha mawalisiano vijiji 49 Dodoma
Mkuu
wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akizugumza na Wakazi wa kijiji
cha Mbori, Kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa wakati wa uzinduzi wa
Mnara wa Matomondo. Aidha Airtel pamoja na USCAF ilizindua minara minne
wilayani hapo na kuwawezesha wakazi katika vijjiji 49 kupata huduma za
mawasiliano ya uhakika.
Meneja
wa Kampuni ya Simu ya Airtel, Mkoa wa Dodoma Paschal Bikomagu
akizugumza na Wakazi wa kijiji cha Mbori, Kata ya Matomondo Wilayani
Mpwapwa wakati wa uzinduzi wa Mnara wa Matomondo. Aidha Airtel pamoja na
USCAF ilizindua minara minne wilayani hapo na kuwawezesha wakazi katika
vijjiji 49 kupata huduma za mawasiliano ya uhakika.
Mkuu
wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri akisalimiana na mchezaji wa timu
ya Manchester United ya Mbori Wilayani Mpwapwa, Juma Athmani katika
mchezo wa fainali iliochezwa juzi katika uwanja wa Ikulu kata ya
Matomondo Wilayani Mpwapwa. Mchezo huo ulikuwa madhumuni kwa ajili ya
uzinduzi wa mnara wa simu wa Matomondo uliojengwa na Kampuni ya simu ya
mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na USCAF ili kufikisha huduma
mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo ya pembezoni mwa nchi.
Manchester ilishinda kwa mabao 4-3 dhidi ya Liverpool.
Mkuu
wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akisalimiana na wachezaji wa timu
ya Liverpool ya Mbori Wilayani Mpwapwa katika mchezo wa fainali
uliochezwa juzi katika uwanja wa Ikulu kata ya Matomondo Wilayani
Mpwapwa. mchezo huo ulikuwa na madhumuni kwa ajili ya uzinduzi wa Mnara
wa simu wa Matomondo,uliojengwa Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa
kushirikiana na USCAF ili kufikisha huduma mawasiliano kwa wananchi
waishio maeneo ya pembezoni mwa nchi. Manchester ilishinda kwa mabao 4-3
dhidi ya Liverpool.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel katika mpango wake wa kufikisha huduma za
mawasiliano kwenye maeneo ya pembezoni imeshirikiana na Mfuko wa
Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwa kujenga na kukamilisha miundombinu ya
mawasiliano katika kata 10 zilizoko katika maeneo ya vijijini ili kutoa
huduma bora ya mawasiliano.
Katika
kufanikisha mkakati huo, Airtel na UCSAF leo imefanya uzinduzi wa
kwanza wa minara minne iliyoko katika kata za Matomondo, Mbuga and Ipera
wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo uzinduzi huo utawawezesha wakazi
zaidi ya 38,000 katika vijiji 49 kuunganishwa na huduma za mawasiliano
toka Airtel na kufurahia huduma na bidhaa mbalimbali ikiwemo huduma za
intaneti, kupiga simu pamoja na huduma ya Airtel money ili kutatua
changamoto zao
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano katika kata ya Matomondo
Dodoma, Meneja wa mauzo wa Airtel Dodoma, Bwn Pascal Bikomagu alisema”
Airtel imejipanga katika kuboresha na kupanua upatikanaji wa huduma za
mawasilino ili kuchochea kukua kwa shughuli za kijamii na kiuchumi
katika maeneo yaliyo na changamoto hususani vijijini
“Kufatia
uzinduzi huu leo tunawashauri wakazi wa kata ya Matomondo na vijiji vya
jirani kutumia huduma za Airtel Money katika kufanya miamala ya
kifedha. Huduma hii ya Airtel Money itawawezesha kutuma na kupokea pesa,
kulipia ankra mbalimbali kwa urahisi na gharama nafuu, na pia kutumiaka
kama mfumo rasmi wa huduma za kifedha kwani upatikanaji wa huduma
zingine za kibenki katika maeneo hayo bado ni changamoto.” Aliongeza
Bikomagu
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mh. Jabir Shekimweli Alisema “
mawasiliano ya simu ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa jamii na
nchi kwa ujumla, nachukua fursa hii kuwahimiza wakazi wa kata za
Ipera,Matomondo na Mbuga kutumia mawasiliano hayo katika kuboresha
shughuli zao za kilimo na biashara ili kuinua kipato.
Naye
Mkuu wa Huduma za Ununuzi na Ugavi UCSAF, John Munkondya alisema
“Tunawapongeza Airtel kwakumaliza ujenzi wa minara hii yakutoa
mawasiliano bora, leo hii tumeanza kuzindua huduma za mawasilino katika
mkoa wa Dodoma. ni matumaini yetu tutaendelea kushirikiana na kuboresha
huduma hizi za mawasiliano ili kuwafika watanzania wengi zaidi.
Airtel
ilisaini makubaliano na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
UCSAF kwa lengo la kufikisha mawasilino katika maeneo ya pembezoni mwa
nchi. Kupitia mpango huu kata 28 nchini zimeweza kufikiwa na hivyo
kuongeza idadi ya minara ya mawasiliano ya Airtel kufikia 2,210 ndani ya
miji zaidi 128 na hivyo kuwafikishia huduma za mawasiliano wakazi zaidi
ya asilimia 85 nchini.
Post a Comment