Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Video: Dayna Nyange adai mastaa wengi hawajui kutongoza ‘wananitongoza lakini hawanishawishi’
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki Dayna Nyange ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, amefunguka na kuzungumzia kiundani kauli yake ambayo amekuwa akitoa kila ...
Msanii wa muziki Dayna Nyange ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, amefunguka na kuzungumzia kiundani kauli yake ambayo amekuwa akitoa kila mara kwamba hawezi kutoka kimapenzi na mastaa wenzake.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Komela’ akiwa amemshirikisha Billnass, amedai anatongozwa na mastaa wengi lakini wanashindwa kumshawishi.
“Sijawahi kudate na staa na si kwamba wakaka wazuri hawapo, na sio kwamba hawanitokei, labda hawajui kutongoza vizuri,” alisema Dayna. “Kwa sababu sijawahi kushawishika kutembea na staa na sipendi kutembea na staa, so wakati mwingine unaweza ukawa haupendi kitu lakini ukashawika kuingia lakini mimi bado hajatokea,”
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya kazi mpya pamoja na kolabo za kimataifa ambazo hakuziweka wazi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top