Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Urusi yasimamishwa kushiriki michuano ya kimataifa ya riadha baada ya kubainika kwa wanamichezo wake
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Nchi ya Urusi imesimamishwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Riadha baada ya kubainika kwa wanamichezo wake kujihusisha na u...


Nchi ya Urusi imesimamishwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Riadha baada ya kubainika kwa wanamichezo wake kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kusisimua misuli.

Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wa Urusi wanaweza kushiriki na kushindana mahali popote endapo wanaweza kukidhi vigezo vya vipimo.
Urusi ilisimamishwa na shirikisho la riadha ulimwenguni I doubel AAF mwezi Novemba mwaka 2015, na wanariadha wake kukosa kushiriki michuano ya Rio Olimpiki ya mwaka jana.
Uingereza wanatarajia kuwa wenyeji wa mashindano ya riadha ya dunia kati ya Agosti 04-13 mwaka huu 2017.
Uamuzi wa kusimamishwa kwa Urusi umefanyika kupitia mkutano mkuu wa Baraza uliofanyika mjini Monaco.
Source: BBC

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top