TID kuiachia ‘Maisha ya Jela’ aliyomshirikisha Fid Q
TID amepanga kuachia wimbo wake uitwao Maisha ya Jela aliomshirikisha Fid Q.
Wimbo huo ulirekodiwa mwaka 2007, siku tatu tu baada ya muimbaji huyo kutoka jela. Kutoka jela kwa muimbaji huyo kulitokana msamaha wa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete siku ya Uhuru.
Maisha ya Jela unazungumzia msoto ambao muimbaji huyo aliupata baada ya kufungwa jela. “TID ameelezea maumivu, maumivu ya moyo, kuchanganyikiwa, na bila kusahau mateso ya kiakili aliyoyapata akiwa jela kutokana na adhabu kali alizozipata baada ya hukumu hiyo,” yanasema maelezo.
Fid Q alikuwa mtu wa karibu na TID wakati wa kifungo na baada ya kutoka na alimwelezea namna wananchi walivyochukulia kufungwa kwake hivyo alikuwa mtu sahihi kushirikishwa kwenye wimbo huo ambao ulikuwa wazo na CEO wa Tongwe Records, J-Murder.
Hata hivyo licha ya wimbo huo kumalizika, haukuweza kutoka kipindi hicho kwasababu walitaka kwanza TID awe kwenye hali ya kawaida baada ya kutoka kifungoni.
Bado haijatajwa tarehe rasmi ya kutoka kwa wimbo huo. Hivi karibuni TID alikiri kuwa mmoja wa waathiriwa wa matumizi ya dawa za kulevya.
Post a Comment