Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Christian Bella: Bongo Fleva ndio imenisaidia kufika hapa
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Christian Bella: Bongo Fleva ndio imenisaidia kufika hapa Mkali wa masauti Christian Bella amedai kuwa muziki wa Bongo Fleva ...

Christian Bella: Bongo Fleva ndio imenisaidia kufika hapa



Mkali wa masauti Christian Bella amedai kuwa muziki wa Bongo Fleva ndio umemsaidia kufika alipo sasa kimuziki.

Muimbaji huyo amesema muziki huo umemsaidia kujifunza vingi na kugundua mapungufu yaliyopo kwenye muziki wa bendi na kutengeneza muziki ambao unaweza kuimba pamoja na mashabiki kwenye matamasha.
“Bongo Fleva ndio imenisaidia zaidi imenifanya mimi kujua natakiwa nifanye nini. Unajua kuna mapungufu tunayo sisi kwenye bendi tunajiimbiaga bila shangwe. Hatuna shangwe kwenye show, nyimbo nzuri watu wanakuangalia na wanacheza, wanakutunza wanakaa lakini kwenye Bongo Fleva nimegundua lazima utengeneze hit inatakiwa mashabiki waimbe, ndio vitu nimejifunza,” amekiambia kipindi cha Dj Sho cha Radio One.
Bella ameongeza kuwa alivyosimama yeye mwenyewe ndio imemlipa zaidi kuliko bendi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top