Rapper Chin Bees amedai kuwa jina lake liliwahi kumfanya Chidi Benz amuambie abadilishe jina ili kutowachanganya watu kutokana na majina yao kuwa na ufanano mkubwa.
Akiongea na Bongo5, Chin amedai kuwa mkanganyiko huo ulitokea katika studio za Mesen Selekta ambapo wote walikuwa wamemshirikisha Ben Pol kwenye nyimbo zao.
“Chid Benz alishawahi kufanya pale wimbo aliomshirikisha ‘Chidi Benz ft Ben Pol, kwahiyo yeye alivyokuja kusearch ngoma alivyoandika tu ile CHI ikaja pale Chin Bees ft Ben Pol, yeye alivyolisoma tu kwa haraka haraka akaona Chidi Benz akaplay, alivyoplay ikaplay ngoma tofauti na yeye mwenyewe aliyokuwa amesikia,” Chin ameiambia Bongo5.
“Oya Mesen huyu nani,” Chin anamnukuu Chidi Benz na Mesen kumwambia kuwa ni Chin Bees. “Ebana wewe sio Chin Bees, wewe ni Kidevu. Kitu ambacho nakumbuka ni kwamba alinishika mguu akanishika na mkono akaninyanyua ‘We sio Chin Beesy ni kidevu.’
Kama hiyo haitoshi, Chin ambaye jina lake ni tafsiri ya Kidevu, amedai kuwa mama yake alidhani kuwa naye alitajwa kwenye orodha ya Makonda baada ya kusikia jina Chidi Benz.
Post a Comment