Waziri Mkuu aagiza idara ya uhamiaji kuandaa semina ya mafunzo ya uraia kwa wahudumu wa hoteli na gesti
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa idara ya uhamiaji kuandaa semina za mafunzo ya elimu ya uraia kwa wahudumu wa hoteli na nyumba za kulala wageni nchini ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo mkoani Njombe ikiwa ni mwanzo wa ziara zake mkoani humo. Aliyasema hayo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo, Ole Sendeka ambapo alitoa taarifa ya mkoa, ambapo idara ya uhamiaji ilibaini taarifa za wahamiaji wa kigeni 119 na wahamiaji haramu 42 ambao walikamatwa huku waziri huyo alisema ni hatari kwa mkoa huo kuwa na wahamiaji wengi wa kigeni.
“Kuwe na utaratibu wa kupitia nyumba za wageni, na wakati mwingine muandae semina muwaite wahudumu wa hoteli na gesti house mnawaita kwenye semina siku moja mbili mna waambia umuhimu wa uraia kwa kuiheshimu nchi yao , uzalendo wao ili waweze kujenga tabia ya mtu yeyote wanae hisi kwamba huyu si mwenyewe,” alisema.
Aliongeza “Wengine wanafanya mazoezi ya kuongea Kiswahili huko katikati ya Rukwa na Tunduma anafanya mazoezi akiona anatosha ndo anaingia huku ndani, anajua hapa kigezo mimi nikizungumza kiswahili mimi ni Mtanzania,lakini Mtanzania ukikaa na mtu aliyejifunza unajua huyu sio mwenyewe,sasa haya wanayajua wenyewe wahudumu wa gesti house na hoteli kwahiyo tengenezeni elimu kwa wale wenzetu ambao watatusaidia kutupa taarifa.”
Post a Comment