Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Trump alalama kuwa wahamiaji haramu ndio waliomnyima kura za wingi (popular votes)
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Trump alalama kuwa wahamiaji haramu ndio waliomnyima kura za wingi (popular votes) Licha ya kuingia Ikulu, Rais Donald Trump anaonekan...

Trump alalama kuwa wahamiaji haramu ndio waliomnyima kura za wingi (popular votes)

Licha ya kuingia Ikulu, Rais Donald Trump anaonekana bado anaumizwa na ukweli kuwa mpinzani wake, Hillary Clinton alimzidi kura za wingi (popular votes), kwenye uchaguzi wa Novemba mwaka jana.

Trump aliyeapishwa wiki iliyopita, alikutana kwenye mkutano wa kwanza na wawikilishi na kudai kuwa mamilioni ya wahamiaji haramu wa Marekani ndio waliomkosesha kura hizo.
Dai hilo ambalo amewahi kulieleza kwenye Twitter limewahi kupingwa vikali kutokana na kutokuwa na ukweli wowote. Trump alipata kura 304 za wachaguaji (electoral college) kumfanya aingie Ikulu huku akiwa nyuma kwa zaidi ya kura milioni 3 za kawaida dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton.
Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, Trump alitumia mkutano huu kujisifia kuhusiana na ushindi alioupata.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top