Timu ya taifa ya Ivory Coast yamkera Jose Mourinho
Kocha wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amechukizwa na timu ya taifa ya Ivory Coast baada ya kumchukua beki Eric Bailey
Bailey ambaye alishiriki katika kikosi cha kwanza cha United katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Middlesbrough na Mourinho alidhani beki huyo atajuimuika na wenzake katika mechi dhidi ya West Ham siku ya Jumatatu.
Mourinho ameuambia mtandao wa klabu hiyo kwamba kocha Michel Dussuyuer alikuwa hayuko tayari kuchukua hatari yoyote wakati wanajiandaa kutetea taji lao la Afrika.
”Baily anaondoka anaenda kuchezea timu yake ya taifa,alisema Mourinho.Ni lazima awe na timu yake mnamo tarehe 2 Januari. Tuliwaomba wamchukue tarehe 3 lakini wakakataa,kwa hivyo hawezi kucheza dhidi ya West Ham”.
Post a Comment