Timu tatu zinaitaka nafasi moja..Nani ataipata?
Kati ya pambano lililokuwa na msisimko mkubwa sana ilikuwa ni kati ya wenyeji Gabon dhidi ya Cameroon.Mchezo huo ulivuta hisia za watu wengi ni kati ya Gabon na Cameroon ambao ulioneshwa moja kwa moja kupitia ZBC2.Katika mchezo huo wenyeji wamefungasha virago huku Cameroon na Burkina Fasso wakifuzu kwa hatua inayofuata.
Leo ni zamu ya Group B ambapo Senegal watacheza na
Algeria huku Tunisia wakikipiga dhidi ya Zimbabwe.Ikumbukwe tayari
Senegal wameshatangulia nusu fainali na matokeo ya aina yoyote leo
hayatawaathiri.Shughuli kubwa iko kwa hizi timu tatu zilizobakia ambazo
ni Tunisia,Zimbabwe na Algeria.Timu zote hizo tatu zinatafuta nafasi
moja iliyobaki kwenda kucheza robo fainali,Algeria na Zimbabwe wana
pointi moja moja huku Tunisia akiwa na pointi tatu.
Algeria wanacheza dhidi ya vinara wa kundi Senegal.Ni
lazima Ageria wawafunge Senegal kama wanataka kufuzu kwa hatua
inayofuat.Ryad Mahrez atakiongoza kikosi hicho kuikabili moja kati ya
timu bora kabisa ya mashindano hayo hadi sasa timu ya taifa ya
Senegal.Ni kazi kubwa kuwafunga na kutokuwazuia wasifunge lakini Algeria
hawana budi na ni lazima wawafunge Senegal ili wafuzu.
Zimbabwe nao wanakutana na Tunisia mwenye alama tatu.Kwa
namna yoyote ili Zumbabwe akae juu ya Tunisia lazima wawfunge huku
wakiomba mabaya kwa Algeria.Zimbabwe amnao mchezo wao wa kwanza
walitakata licha ya kutoka sare na Algeria lakini mchezo wao wa pili
walitepeta kwa Senegal.
ZBC2 chaneli namba 116 katika Azam Tv ndio sehemu ambapo utapata jibu kamili la yupi anakwenda na yupi anabaki.
Post a Comment