MOUNT MERU RICKERNEST MUSIC BAND YAJA KWA KASI JIJINI ARUSHA, YAAHIDI KUFANYA MAPINDUZI YA MUZIKI WA DANSI NCHINI
Bendi
mpya ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mount Meru Ricknest
music bandi imezinduliwa rasmi mkoani Arusha ikiwaahidi wapenda
mziki wa dance burudani isiokuwa na mpinzani.
Akiongea
na waandishi wa habari jana mmoja wa wakurugenzi wa bendi hiyo Ernest
mlolere alisema kuwa kwa sasa wameitambulisha bendi hiyo kwa wakazi wa
mkoa wa Arusha tu na wanatarajia kuzindua bendi hiyo rasmi katika siku
ya wapendanao (valentine day ) hapa hapa jijini Arusha.
Alibainisha
kuwa bendi hiyo ipo chini ya wakurugenzi watatu akiwemo yeye mwenyewe
Ernest Mlolere, Denis Kaiza pamoja na Prisca Aloyce ambapo wamekaa
chini na wakaamua kuanzisha bendi hiyo ili kuweza kuwapa burudani
wakazi wa mkoa wa Arusha ambao wamekuwa wakikosa burudani ya bendi ya
uhakika kwa muda mrefu.
Alisema
kuwa kumekuwa na bendi jijini hapa lakini zimekuwa hazikoshi nyoyo za
wapenzi wao wa musiki wa dance hivyo wameona wawaletee wanamusiki wenye
uzoefu, wenye vipaji vya kutosha ili wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja
na jirani kuweza kupata burudani.
Aidha
aliongeza kuwa bendi hii haitakaa Arusha tu bali itakuwa inatembea
mikoa mbalimbali ili kuwapa burudani wapenzi wa music wa dance wa nchi
nzima.
“Tumejipanga
vyema. Tunaweza na tuna uhakika ujio wa bendi hii utawafurahisha na
kuwashika wapenzi wengi wa music wa dance kwani wanamuziki ambao wapo
katika bendi hii ni wazuri na wana vipaji vya kutosha. Nadhani unajua
kabisa ukiwa na kitu kizuri lazima watu wakipendi naamini kabisa wetu
wapenzi wa bendi watawapenda.
Alibainisha
kuwa katika bendi hii pia kuna wana music kutoka katika bendi maarufu
za nje ambapo alitaja baadhi ya wanamusic waliotoka katika bendi za nje
kuwa ni pamoja na rais wa bendi Fabrice Kinyenya (kulialia) ambapo yeye
ametoka katika bendi ya Ferre Gola pamoja na Katoto (Tanesco) ambaye
yeye ametoka katika bendi ya Fally Ipupa nchini DRC.
Aliongeza
kuwa wanajua kabisa kuna bendi zilizotangulia hapa nchini na
zinaaminika ila kwa jinsi walivyojipanga yeye na wanamuziki wake ana
imani kabisa watazipita bendi zote zilizopo hapa nchini na hata zile
zilizoanzishwa hivi karibuni zilizopo jijini hapa.
“Sasa
hivi tupo katika harakati za kupanga siku ya uzinduzi rasmi wa bendi
hii ila hii leo tumekuja kuwaonjesha wakazi wa mkoa wa Arusha kuwa kuna
bendi inayopiga vizuri sana iliopo hapa mkoani kwao. Na kwa kuwa ni
nyumbani tumejipanga kila siku ya Jumamosi kuwapa burudani ambapo
tutakuwa tunapiga katika ukumbi wa Triple A”, alisema Mlolere.
Kwa
upande wake Rais wa bendi hiyo Fabrice Kinyenya (Kulialia) alisema kuwa
wamejipanga vilivyo kuwapa wapenzi wa musiki wa dance burudani ya
uhakika ambayo itamkosha kila mtu nyoyo.
“Mimi
sipendi kuongea sana. Napenda kufanya vitendo zaidi. Wasanii wangu wapo
vizuri na nachosema tu ni kuwa wapenzi wa musiki wa dance wasubiri
kupata burudani ya nguvu yenye viwango vya kimataifa. Hapa ni kazi tu
hakuna maneno mengi “alisema Fabrice.
Alisema
kuwa hadi sasa wameshatunga nyimbo za bendi na watazitambulisha siku
ambayo bendi itazinduliwa rasmi, akibainisha kuwa bendi hiyo ina nyimbo
nzuri ambazo zitamfurahisha kila mtu.
Hii ni
bendi ya tatu kuzinduliwa ndani ya jiji la Arusha kwani kabla ya hii
kipindi cha mwaka uliopita 2016 bendi mbili zilianzishwa jijini hapa
ambapo bendi ya kwanza ya ikiwa mjengoni music band, na pia kuna bendi
ya East Afrika music bandi zote zikiwa ni bendi za musiki wa dance.
Hivyo
wakazi wa jiji hili wamenufaika kwa kuletewa muziki wa ladh tofauti na
kipindi cha nyuma ambapo wakazi wa jiji hili walikuwa wakipata taabu
sana kupata burudani ya muziki wa live band.
Rais wa bendi ya Mounti Meru Rickernest Music Band Fabrice Kinyenya (kulialia) Akiwa anaimba katika usiku wa kuwatambulisha bendi hiyo wakazi wa jiji la Arusha
wanamusiki
wa bendi ya Mounti Meru Rickernest Music Band wakiwa wanaonyesha
kiwango chao ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha
waimbaji wa bendi ya Mounti Meru Rickernest Music Band wakiwa fanya yao
Wanenguaji wa bendi ya Mount meru Rickernest Music Band wakifanya yao
Rais wa bendi akifanya mambo ndani ya ukumbi wa Triple A
Wa
kwanza kulia ni mmoja wa wakurugenzi wa bendi ya Mount meru
Rickernest Music Band Akifatilia onyesho, wa pili kushoto ni mkurugenzi
mwingine wa bendi hiyo Prisca Aloyce wote wakiwa wanafatilia kwa makini
onyesho.
Post a Comment