Barnicoz Tech Barnicoz Tech Author
Title: Ashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi na kutaka kumfukia
Author: Barnicoz Tech
Rating 5 of 5 Des:
Ashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi na kutaka kumfukia Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindi...

Ashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi na kutaka kumfukia


Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindisa (29) mkazi wa Mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangano, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Athanasi Malindisa(70) na kuchimba shimo kutaka kumfukia.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji.
Akizungumza mjini hapo mmoja wa wanafamilia ambaye ni mdogo wa marehemu Pius Malindisa, alisema walipata taarifa ya kifo cha ndugu yao Januari Mosi mwaka huu saa 1:30 jioni kutoka kwa mtoto wa marehemu Patrick Malindisa.
Alisema marehemu alikuwa akiishi na mtoto wake huyo ambapo baada ya kufanya mauaji hayo alianza kuwaarifu ndugu kuwa amefariki kwa ugonjwa wa tumbo.
Kutokana na taarifa hizo ndugu walikusanyika nyumbani kwa marehemu ambapo baada ya kuingia ndani walikuta akiwa amelala ndipo walipowaita viongozi wa mtaa na baada ya kufunua walibaini marehemu ameuawa kwa kupigwa na kitu kichwani na kidevuni.
“Tulipofika hapa tulikuta shimo limechimbwa ndani ya nyumba na inaelekea lilimshinda na kuamua kuanza kutoa taarifa kwetu ambapo alidai alikuwa anaumwa ugonjwa wa tumbo,” alisema Pius.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji alithibisha kutokea kwa tukio hilo alisema kuwa, “Baada ya kuuangalia mwili wa marehemu tulikuta majeraha kichwani pamoja na kwenye kidevu,jeraha ambalo limesababishwa na kitu chenye ncha butu, lakini uchunguzi wa awali inaonyesha marehemu alikuwa anaishi na mtoto wake aitwaye Patrick Malindisa (29), uchunguzi unaonyesha kuwa mtoto huyu awali alienda kumuona baba yake mdogo ambapo alienda kumueleza kuwa huyu baba yake mzazi ambaye ni marehemu kamuona yupo chumbani kwake analalamika mauvimu lakini maumivu ya tumbo,”alisema Kamanda Mwombeji.
“Polisi walipofanya uchunguzi walibaini kuwa kifo hicho sio cha kawaida ni cha kipigo, walimchukua kijana huyo kwaajili ya mahojiano kulingana na utata wa maelezo hayo kwamba marehemu alikuwa na matatizo ya kuumwa na tumbo wakati huo alikuwa na majeraha mwilini.”

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top