SHINDANO LA FREESTYLE FOOTBALL KWA VIJANA KUANZA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 19, 2016
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MASHINDANO
ya kuchezea mpira (Football Freestyle) yaliyoandaliwa na chama cha
mchezo huo Freestyle Football Tanzania (FFT) yanatarajiwa kuanza Novemba
19 kwa Wilaya tatu za Jiji la Dar es Salaam Temeke, Ilala na Kinondoni
na uzinduzi wa shindano hilo unatarajiwa kuanzia kwenye viwanja vya
Mwembe Yanga.
Mgeni
rasmi kwenye uzinduzi huo unayodhaminiwa na kinywaji cha Red bull
ikishirikiana na Clouds TV kupitia kipindi cha Sports Bar anatarajiwa
kuwa Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea.
Akizungumza
na Mratibu wa shindano hilo Jacob Mbuya amesema kuwa washiriki wa
shindano hilo watajiandikisha bure na washiriki wanatakiwa kuwa na umri
kuanzia miaka 15 na kuendelea huku fomu
za ushiriki zinapatikana Clouds TV na Ofisi za chama hicho zilizopo
Kinondoni pamoja na mitandao ya kijamii kupitia kurasa zao.
Mashindano
yanatarajiwa kuanzia Wilaya ya Temeke Novemba 19 na kutapatikana
washiriki watano na baadae kuhamia kwenue wilaya ya Ilala ambayo pia
itatoa washiriki watano huku Kinondoni ikitoa sita ambao wataingia
Fainali itakayochezwa Coco Beach, Disemba 11 na kwa
upande wa Wilaya ya Ilala shindano hilo litafanuyika kwenye viwanja
vya Boma, Novemba 26 kabla ya kuelekea Kinondoni kwenye uwanja wa Tp
Sweet Corner, Disemba 3. Rais wa Freestyle
Football Tanzania (FFT) Pascal Chang'a amesema kuwa wameamua kuanza
kufanya mashindano haya na kupata vipaji ambao watawapa fursa ya kwenda
kimataifa zaidi kwani huwezi kwenda kushiriki kama hujafanya nchi kwako
na alitaja baadhi ya
sheria za mchezo huo kuwa ni kila mshiriki atapewa sekunde 30 za
kuchezea mpira, mchezaji atakuwa peke yake jukwaani na pia akidondosha
mpira atakuwa amepoteza pointi.
Naye
Afisa Masoko wa Mahans Oysterbay Drinks, Hanson Heddy amesema kwua
wameamua kushirikiana na FFT ili kuweza kuibua vipaji vya vijana katika
mchezo huu na pia wao wamedhamini kwa kila kitakachokuwa kinahitajika.
Katibu
wa Freestyle Football Tanzania (FFT) Morisson Nossey akizungumza na
waandishi wa habari wakati kuhusiana na mashndano ya kuchezea mpira
yanayotarajiwa kuanza Novemba 19, kushoto ni Afisa Masoko wa Mahans
Oysterbay Drinks, Hanson Heddy na kulia ni Mratibu wa Shindano hilo Jacob
Mbuya.
Mratibu wa
Shindano la kuchezea mpira Freestyle Football Jacob Mbuya akizungumza na
waandishi wa habari na kutoa utaratibu wa ushiriki kwa vijana kuanzia miaka 15
na kuendelea kulia ni
Katibu wa Freestyle Football Tanzania (FFT) Morisson Nossey
kushoto ni Afisa Masoko wa Mahans Oysterbay Drinks, Hanson Heddy na
mwisho ni Rais wa Freestyle Football Tanzania (FFT) .



Post a Comment