Serekali yateuwa waratibu uwezeshaji wa wizara
Serekali
imewataka Waratibu wa Uwezeshaji wa Wizara walioteuliwa kuwa watendaji
makini ili kusaidia kamati zao za uwezeshaji wananchi kufuatilia kwa
ukamilifu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
ya Mwaka 2004 na kuchangia kuandaa takwimu za uchumi wa taifa.
Akifungua
mafunzo ya siku tatu ya Wenyeviti wa Kamati za Uwezeshaji na Waratibu
wa Uwezeshaji, mjini hapa jana, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,
Vijana na Ajira Anthony Mavunde, amesema kuwa sababu ya serekali kuwa
na kamati na waratibu hao ni kupata watendaji wa kutumikia Watanzania
kwa kuwawezesha, kuwasaidia kumiliki kikamilifu na kunufaika na uchumi
wa taifa katika mazingira ya sasa.
Waziri
huyo ameliita suala la uwezeshaji wananchi kuwa ni ajenda muhimu ya
taifa na kutaka zikusanywe takwimu za kuridhisha juu ya ukuwaji wa
uchumi katika miaka na jinsi wananchi wanavyonufaika na ukuwaji huo.
Amesisitiza “..haitakuwa na maana kama ukuwaji wa uchumi hauwanufaishi
wananchi walio wengi na (pia kama) hazipo takwimu za kuridhisha za
ukuaji wa chumi.”
Akisisitiza
umuhimu wa ufuatiliaji, waziri amesema maeneo ya kupwewa kipaumbele ni
kujua ni kiasi gani Watanzania wanashiriki na kunufaika kutokana na
uwekezaji mkubwa unaofanywa hapa nchini na makampuni ya kigeni katika
sekta mbali mbali.
Amewataka
watendaji kulisaidia taifa “kubainisha vikwazo au sababu zinazokwamisha
Watanzania kushiriki katika uwekezaji, ikiwa ni pamoja kupata zabuni za
kutoa huduma mbali mbali katika makampuni hayo na pia kupata nafasi za
ajira.”
Bw
Mavunde amesema serekali inafanya kazi kwa bidii kuleta maendeleo ya
haraka kwa Watanzania. Na kuongeza kuwa kwa vile utekelezaji wa majukumu
ya uwezeshaji unafanyawa na wadau wa sekta za umma na binafsi,
matarajio ya serekali ni kuona kamati za uwezeshaji na madawati ya
uwezeshaji katika wizara, idara, taasisi za serekali, mikoa na
halmashauri zinafanya kazi kwa karibu na kila mudau.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i
Issa, amesema baraza linatarajia kila wizara, idara na taasisi ya
serikali kutoa mchango wake katika kutekeleza sera ya uwezeshaji
wananchi.
Amesema
mafunzo yameandaliwa ili kuliwezesha baraza kupata maoni juu ya mambo
wa msingi kwani washiriki watagusia makujumu na programu zinazotekelezwa
na NEEC, mkakati wa uwezeshaji na mwongozo wa utekelezaji wake, wajibu
na majukumu ya kamati na waratibu wa madawai ya uwezeshaji, miongozo ya
kuwasilisha taarifa za uwezeshaji, mifuko ya uwezeshaji na programu za
mitaji, ushiriki wa Watanzania kwenye uwekezaji (local content) na
rasimu ya mapitio ya sera ya taifa ya uwezeshaji.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole
Gabriel, ambaye ni mshiriki amesema mafunzo yatawapa uwelewa mpana wa
namna ya kuwahudumia wananchi katika wizara, hasa katika kutekeleza sera
ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Mwenyewe, ameongeza, “nimejifunza mambo mengi sana leo. Nimefahamu kwa undani majukumu ya baraza na muundo wake.”
Baadhi ya
Wenyeviti wa Kamati za Uwezeshaji na Waratibu wa Uwezeshaji
wakifuatilia mafunzo ya siku tatu ya Wenyeviti wa Kamati za Uwezeshaji
na Waratibu wa Uwezeshaji, mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo wa
uwelewa na wajibu wao katika Wizara, Idara na Taasisi wanazotoka,
mafunzo hayo yalifunguliwa jana Mkoani Morogoro na Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde
((katikati) akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya
Wenyeviti wa Kamati za Uwezeshaji na Waratibu wa Uwezeshaji, mafunzo
yenye lengo la kuwajengea uwezo wa uwelewa na wajibu wao katika Wizara,
Idara na Taasisi mbalimbali wanazotoka (kulia) ni Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel,
(kushoto) ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (
NEEC) Bi. Beng’i Issa.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde
(kushoto) akimsikiliza kwa makini ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel ( kulia) muda
mfupi mara baada Naibu Waziri huyo fungua mafunzo ya siku tatu ya
Wenyeviti wa Kamati za Uwezeshaji na Waratibu wa Uwezeshaji, mafunzo
yenye lengo la kuwajengea uwezo wa uwelewa na wajibu wao katika Wizara,
Idara na Taasisi wanazotoka, Morogoro jana, (katikati) ni Katibu
Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ( NEEC) Bi. Beng’i
Issa.

Post a Comment