PENATI YAWAPA USHINDI YANGA WA GOLI 1,0 DHIDI YA TANZANIA PRISON MBEYA....
Saimon
Msuva Akitimuwa Vumbi kwa shuti kali wakati akipiga penati katika lango
la Tanzania Prison na kuipatia yanga goli moja kwa bila katika mchezo
ulio chezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya Ikiwa ni muendelezo wa
Ligi Kuu Ya Soka Vodacom Tanzania Bara.
TIMU
ya Yanga imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya askari
magereza wa mkoani Mbeya Tanzania Prisons na ku�kisha jumla ya alama 30
wakiwa nyuma ya alama tano dhdi ya Mahasimu wao wakubwa Simba ambao
wamepoteza mchezo wao wa leo. Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa
Sokoine ulikuwa wa kasi na kila upande ukicheza kwa umakini uliweza
kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza huku kila timu ikiwa haijaona
lango la mwenzake. Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya
mabadiliko na kuanza kulisakama lango la Tanzania Prisons lakini makosa
ya washambuliaji wa timu hiyo walishindwa kutumia nafasi hizo na kukosa
magoli, lakini makosa ya mabeki wa Yanga yalisabababisha Prisons kupata
penati lakini uwezo wa golikipa Beno Kakolanya aliweza kuokoa mkwaju
huo. dakika ya 74 mwamuzi wa kati Hance Mabena kutoka Tanga anaipatia
Yanga penati inayopigwa na Simon Msuva na kuiandikia Yanga goli la
kuongoza na mpaka dakika 90 za kumalizika kwa mchezaji huo.
Kutoka
Shoto ni Haruna Niyonzima wa Timu ya Yanga Akimuomba Radhi Mchezaji
Mwenzie Wa Timu ya Yanga Saimon Msuva Pindi alipokuwa Akijibizana Na
Muamuzi.
Victor Hangaya Shoto Akimpoteza Deus Kaseke.
Kutoka
Shoto ni Benjamin Asukile akichuwana Vikali na Mwinyi Haji katika
mtanange wa Yanga na Tanzania Prison ulio chezwa Katika Uwanja wa
Sokoine Jijini Mbeya.
PICHA NA MR.PENGO MAELEZO ZAINAB NYAMKA MMG.











Post a Comment